insiderbux
insiderbux
English Ingia Pakua app

App ya simu + web app · akaunti moja

Endesha biashara yako yote sehemu moja.

Mauzo, matumizi, stoo, wateja, pesa, hesabu na kodi. Rekodi kwenye simu ukiwa kaunta, simamia kwenye web ukiwa ofisini, na uone kila shilingi inavyotembea.

Pakua kwenye App Store Ipate kwenye Google Play
Fungua web app
insiderbux kwenye simu na laptop

Mauzo

Rekodi mauzo kwa sekunde.

Chagua bidhaa, pokea keshi, mobile money, benki au mkopo. Risiti au invoice safi inaenda kwa WhatsApp, na malipo kidogo kidogo yanafuatiliwa mpaka yaishe.

Pesa

Jua kila shilingi iko wapi.

Keshi, benki na mobile money kila moja na balance yake halisi. Kuhamisha pesa, pesa iliyoingia na iliyotoka, vyote vinajumlishwa vyenyewe.

Stoo

Stoo inajihesabu yenyewe.

Kila mauzo na manunuzi yanasogeza stoo. Scan barcode kwa kamera, pata tahadhari kabla bidhaa haijaisha, na ujue rafu zako zina thamani gani.

Hesabu na kodi

Hesabu tayari TRA wakiuliza.

Faida na hasara, balance sheet na cash flow zinatoka kwenye ulichorekodi. VAT return na tarehe za kufaili zinaonekana mapema, na kikumbusho.

Kwa siku ndefu za kazi

Rahisi kwa macho. Imefungwa kwa wengine.

Mwanga na giza, PIN ya app kulinda hesabu zako, two-step sign-in, na Kiswahili au Kiingereza kwenye kila skrini.

Web app

Na web app kamili kwa ofisi.

Akaunti ile ile kwenye skrini kubwa: table pana, fomu za pembeni, ku-import data na kufunga mwezi, kwa kazi zinazohitaji nafasi.

Fanya kazi haraka

Table kubwa. Fomu za haraka.

Chuja maelfu ya mauzo, rekodi bili yenye vitu vingi kwenye fomu moja, pokea malipo na tuma statement bila kuhama ukurasa.

Uhasibu halisi

Ripoti ambazo mhasibu wako ataziamini.

Double-entry halisi nyuma ya pazia: chart of accounts, trial balance, assets na depreciation, mtaji na mikopo, na ukaguzi wa hesabu unaoonyesha chochote kisichokaa sawa.

Pamoja muda wote

Uza kwenye simu. Ona kwenye web.

Mabadiliko yanaonekana kwenye simu na web ndani ya sekunde, kwa kila tawi na kila mtu wa timu yako.

insiderbux kwenye simu na laptop

Imetengenezwa kwa jinsi biashara za Tanzania zinavyofanya kazi.

  • Shilingi na mobile money

    TZS kila mahali, na M-Pesa, Airtel Money, Mixx by Yas na benki kama akaunti halisi za pesa.

  • TRA, VAT na tarehe

    VAT return kama umesajiliwa tu, hata miezi isiyo na mauzo, na kalenda ya kila tarehe ya kufaili.

  • Kiswahili na Kiingereza

    Kila skrini kwa lugha zote mbili, kwa Kiswahili cha wafanyabiashara, sio cha kitabuni.

  • Simu yoyote, skrini yoyote

    Android, iPhone na web, kwa akaunti moja na hesabu moja.

Imepangwa kwa aina ya biashara yako.

Chagua aina ya biashara yako, insiderbux inapanga stoo, menyu na chart of accounts kulingana nayo.

Duka la rejarejaMauzo ya haraka, stoo rahisiJumlaMauzo makubwa na wateja wa mkopoMgahawa na baaChakula, vinywaji na mapato ya sikuFamasiBatch na tarehe za kuishaHardwareVifaa vya ujenzi na zanaBiashara ya mazaoMazao, magunia na jumlaKiwandaMalighafi na bidhaa tayariElectronicsSimu, accessories na matengenezoHudumaKazi na invoiceHoteli na lodgeVyumba na hudumaDuka la rejarejaMauzo ya haraka, stoo rahisiJumlaMauzo makubwa na wateja wa mkopoMgahawa na baaChakula, vinywaji na mapato ya sikuFamasiBatch na tarehe za kuishaHardwareVifaa vya ujenzi na zana
Biashara ya mazaoMazao, magunia na jumlaKiwandaMalighafi na bidhaa tayariElectronicsSimu, accessories na matengenezoHudumaKazi na invoiceHoteli na lodgeVyumba na hudumaDuka la rejarejaMauzo ya haraka, stoo rahisiJumlaMauzo makubwa na wateja wa mkopoMgahawa na baaChakula, vinywaji na mapato ya sikuFamasiBatch na tarehe za kuishaHardwareVifaa vya ujenzi na zanaBiashara ya mazaoMazao, magunia na jumlaKiwandaMalighafi na bidhaa tayariElectronicsSimu, accessories na matengenezoHudumaKazi na invoiceHoteli na lodgeVyumba na huduma

Kila kitu biashara inachohitaji.

Anza na mauzo na matumizi. Washa zaidi ukikua.

Kila module hesabu zako zinahitaji.

Vyote kwenye akaunti moja. Kila plan inawasha zaidi.

Pesa inayoingia na kutoka

  • Mauzo na invoice
  • Risiti
  • Matumizi na bili
  • Manunuzi
  • Wateja
  • Ma-supplier
  • SMS za kukumbusha malipo
  • Madeni ya kudai na kudaiwa

Stoo

  • Stoo
  • Catalogue na bei
  • Kuscan barcode
  • Batch na expiry
  • Arifa za stoo kuisha
  • Thamani ya stoo
  • Kunakili kwenda tawi lingine

Hesabu

  • Keshi na benki
  • Mtaji na mikopo
  • Assets na depreciation
  • Chart of accounts
  • Trial balance
  • Ukaguzi wa hesabu
  • Opening balances
  • Mwaka wa fedha

Ripoti na kodi

  • Faida na hasara
  • Balance sheet
  • Cash flow
  • VAT return
  • Kalenda ya kodi
  • Excel
  • PDF na print

Timu na zana

  • Wafanyakazi na majukumu
  • Matawi
  • Shughuli na arifa
  • Import
  • Two-step sign-in
  • PIN ya app
  • AI ya kusoma risiti
  • Msaidizi wa AI

Plan rahisi kwa shilingi za Kitanzania.

Lipia ndani ya app kwa mobile money. Anza bure, hakuna kadi.

Maswali

Kweli insiderbux ni bure?

Ndiyo. Plan ya Free haina muda wa kuisha na inatosha mauzo na matumizi ya biashara ndogo kwa mwezi. Plan za kulipia zinaongeza rekodi, wafanyakazi na zana za hesabu.

Lazima nijue uhasibu?

Hapana. Unarekodi mauzo na matumizi kama unavyofanya kawaida. insiderbux inapanga hesabu kamili nyuma ya pazia, tayari kwa mhasibu wako.

Inafanya kazi kwa Kiswahili?

Ndiyo. Kila skrini kwenye simu na web iko kwa Kiswahili na Kiingereza. Badilisha muda wowote kwenye settings.

Wafanyakazi wanaweza kuitumia bila kuona kila kitu?

Ndiyo. Alika wafanyakazi na uchague kila mtu anaona nini na anaweza kufanya nini, tawi kwa tawi.

Data yangu iko salama?

Data yako ni ya kampuni yako tu. Kuingia kunaweza kutumia two-step verification, na app ya simu inaweza kufungwa kwa PIN.

Naweza kutumia kwenye kompyuta?

Ndiyo. Ingia kwenye web kwa akaunti ile ile. Kila kitu kinakaa sawa na simu.

Biashara yako, kwa mpangilio. Kuanzia leo.

Bure kwenye Android na iPhone. Data yako inakufuata hadi kwenye web.

Pakua kwenye App Store Ipate kwenye Google Play
Scan kupakua

Pia kutoka insider

Tools tunazotengeneza kwa biashara maalum. Umakini ule ule, hesabu zile zile za Tanzania, na undani zaidi pale biashara inapohitaji.

Kaffekaffe.insider.co.tz

Kahawa, kuanzia mnadani hadi gunia linalouzwa.

Imejengwa kwa wafanyabiashara na viwanda vya kahawa: nunua moja kwa moja au kwenye mnada wa TCB, pokea kwa uzito na unyevu kwenye maghala, pitisha work order kwenye kukoboa, kusafisha na kupanga madaraja, hamisha stoo kati ya matawi na uuze kahawa iliyokamilika. Benki, mali, viwango vya fedha na ukaguzi wa TRA vimo ndani.

  • Manunuzi na mnada wa TCB
  • Maghala kwa uzito
  • Work order za uchakataji
  • Uhamisho kati ya matawi
  • Benki, mali na viwango vya fedha
Tembelea Kaffe